Uncategorized

YONDANI BEKI KISIKI HUYO NAMUNGO

admin September 20, 2020 2:47 pm

 


KELVIN Yondani beki kisiki aliyekuwa anakipiga ndani ya Yanga msimu uliopita inaelezwa kwa sasa ni mali ya Namungo FC ambayo inashiriki michuano kimataifa.


Namungo inayonolewa na Kocha Mkuu, Hitimana Thiery inaiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kuwa washindi wa pili wa fainali ya Kombe la Shirikisho ambalo limechukuliwa na Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara.


Taarifa kutoka mtu wa ndani ya Namungo FC zimeelza kuwa ulikuwa ni mpango mrefu kuipata saini ya beki huyo ambaye alishindwana na Yanga kwenye masuala ya mkataba.


“Ilikuwa muda mrefu hesabu za kumpata beki huyo ila kuna mambo hayakukamilika kwa kuwa ni mchezaji huru taratibu za mwisho zikikamilika kila kitu kitawekwa wazi,” ilieleza taarifa hiyo.


KIKOSI CHA SIMBA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA BIASHARA UNITED KIKOSI CHA BIASHARA UNITED KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply