Uncategorized

MALENGO YA DODOMA JIJI NI KUSEPA NA TAJI LA LIGI KUU BARA

admin September 26, 2020 11:47 am

 


UONGOZI wa Dodoma Jiji FC inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara umesema kuwa malengo yao makubwa ni kutwaa ubingwa kwa msimu wa 2020/21 hivyo watapambana kushinda kwenye mechi zao zote watakazocheza.


Leo Dodoma Jiji itakuwa kibaruani muda mfupi kuanzia sasa mbele ya Polisi Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.


Mchezo huo unatarajiwa kuanza kutimua vumbi majira ya saa 8:00 mchana ni wa mzunguko wa nne ndani ya ligi.

Katibu Mkuu wa Dodoma Jiji FC, Johnson Fourtnatus amesema: “Mikakati yetu ni kumaliza katika nafasi tatu za juu kwenye msimamo kwa msimu huu hivyo kila mchezo kwetu ni fainali kwa maana hiyo tutaingia uwanjani tukiwa tunajua tunaenda kupambana na timu nzuri.


“Pia lengo lengo letu ni kuona kwamba tunafanikiwa  kuchukua ubingwa basi hawa wapinzani wetu leo hatutawaonea huruma.”

 

GWAMBINA YATUMA UJUMBE HUU SIMBA KOCHA SIMBA KUIFUATA GWAMBINA FC KWA TAHADHARI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply