Uncategorized

COASTAL UNION YAAMBULIA POINTI TATU KWA MARA YA KWANZA VPL

admin September 28, 2020 5:47 pm


 COASTAL Union inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda leo Septemba 28 imesepa na pointi tatu kwa mara ya kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara baada ya kucheza mechi tatu ambazo ni dakika 270 bila kuambulia ushindi zaidi ya sare.

Bao pekee la ushindi kwa Coastal Union lilipachikwa dakika ya 87 baada ya mabeki wa JKT Tanzania kujichanganya kuokoa hatari ambapo Edson Katanga alijifunga dakika ya 87.


Mchezo wa kwanza Coastal Union ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Namungo kisha ikapoteza kwa kufungwa mabao 2-0 mbele ya Azam FC na ililazimisha sare ya bila kufungana na Dodoma Jiji, Uwanja wa Mkwakwani.


Leo imeibukia mbele ya JKT Tanzania ambaowamewapa zawadi ya ushindi wa pointi tatu kwa mara ya kwanza. Safu ya ushambuliaji ya Coastal Union bado haijaambulia bao ndani ya dakika 360.


Ushindi huo unaifanya Coastal Union kufikisha jumla ya pointi 4 ikiwa nafasi ya 14 huku JKT Tanzania ikiwa nafasi ya 13 na pointi nne wakitofautiana kwenye idadi ya mabao ya kufunga na kufungana.


Mchezo wa leo ulikuwa ni wa mwisho kukamilisha mzunguko wa nne ambao ulikuwa ni wa ushindani mkubwa na umeshuhudia bao moja la leo la kujifunga ndani ya dakika 90.

COASTAL UNION YAAMBULIA POINTI TATU KWA MARA YA KWANZA VPL MZUNGUKO WA NNE ULIKUWA MOTO, MABAO 13 YAKUSANYWA, MBABE WAO NI KAHEZA NA KISSU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply