Uncategorized

KAGERA SUGAR YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA YANGA

admin September 18, 2020 12:47 pm


 UONGOZI wa Kagera Sugar umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho utakaowakutanisha mbele ya Yanga, Uwanja wa Kaitaba.


Kagera Sugar itamenyana na Yanga ikiwa imetoka kulazimisha sare ya bila kufungana mbele ya Gwambina FC kwenye mchezo wao uliopita huku Yanga ikitoka kushinda bao 1-0 mbele ya Mbeya City.


Mecky Maxime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa maandalizi yapo sawa na kila kitu kinakwenda vizuri.


“Kila kitu kipo sawa nasi tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu ujao.Ushindani ni mkubwa hilo lipo wazi lakini tunahitaji kupata matokeo.


“Tunajua kwamba utakuwa mchezo mgumu lakini tutapambana kupata matokeo chanya, mashabiki wajitokeze kuona ushindani utakavyokuwa pamoja na burudani,” amesema.


Mchezo huo utakaopigwa Septemba 19 utakuwa wa kwanza kwa Yanga kucheza nje ya Dar kwa msimu wa 2020/21 huku ukiwa ni wa pili kwa Kagera Sugar kucheza nyumbani.



KOCHA SIMBA ATAJA SABABU YA WACHEZAJI WAKE KUJENGA USHKAJI NA BENCHI KAGERA SUGAR YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply