Uncategorized

KOCHA MANCHESTER UNITED: TULISTAHILI USHINDI

admin October 21, 2020 6:47 am


OLE Gunnar Solskjaer, Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa walistahili ushindi usiku wa kuamkia leo mbele ya PSG kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati wakiibamiza mabao 2-1 PSG.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Parc des Prinnces jumla yalifungwa mabao matatu yote yalifungwa na wachezaji wa timu ya Manchester United.

Bruno Fernandes alianza kufunga bao la kwanza dakika ya 23 kwa mkwaju wa penalti likasawazishwa na Anthony Martial aliyejifunga dakika ya 55 na nyota wa mchezo huo Marcus Rashford alifunga bao la ushindi dakika ya 87.

Solskjaer ambaye alianzisha kikosi chake bila nahodha Harry Maguire alimuweka pia benchi kiungo Paul Pogba amesema kuwa anahisi vizuri kwa timu yake kushinda na walistahili kupata ushindi huo.


“Najihisi vizuri na nina furaha kwa timu kushinda, wachezaji wote walitambua kwamba wana kazi ngumu ya kufanya na hawajaniangusha, wanastahili pongezi katika hili,” amesema.

MUZIKI WA TANZANIA PRISONS WAIPA PRESHA SIMBA MATOKEO YA MECHI ZA JANA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply