Uncategorized

KAZI TATU ZA MOTO KWA YANGA KANDA YA ZIWA HIZI HAPA

admin October 25, 2020 3:47 am

 


CEDRICK Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga ana kazi ya kumalizana na timu tatu za kanda ya ziwa kusaka pointi tisa kutoka kwa timu ambazo atakutana nazo uwanjani.


Mchezo wake wa kwanza, Kaze aliweza kusepa na pointi tatu mbele ya Polisi Tanzania kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Uhuru Oktoba 22 baada ya kupokea mikoba ya Zlatko Krmpotic aliyefutwa kazi Oktoba 3.

Yanga ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 16 baada ya kucheza mechi sita za ligi.

Leo Oktoba 25 ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya KMC Uwanja wa CCM Kirumba. KMC  yenyewe ipo nafasi ya sita ikiwa na pointi 11 baada ya kucheza mechi saba.

Oktoba 30 kete yake itakuwa ni dhidi ya Biashara United iliyo nafasi ya nne na pointi 13 baada ya kucheza mechi saba, Uwanja wa Karume, Mara.


Novemba 3 atamaliza ziara yake kwa kumenyana na Gwambina iliyo nafasi ya 10 na pointi 9,Uwanja wa CCM Kirumba.

OKTOBA 25, LIGI KUU BARA RATIBA IPO HIVI LEO COASTAL UNION: TUMEADHIBIWA KWA MAKOSA YETU WENYEWE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply