LIGI Kuu Tanzania Bara kwa sasa ipo mzunguko wa nane ambapo leo Oktoba 25 kazi ni moja tu kwa timu kuingia uwanjani kusaka pointi tatu muhimu.
Polisi Tanzania iliyo nafasi ya saba na pointi 11 v Biashara United, iliyo nafasi ya nne na pointi 13 saa 8:00 mchana. Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Mwadui FC iliyo nafasi ya 12 na pointi tisa v JKT Tanzania, iliyo nafasi ya 12 n pointi tano saa 10:00 jioni. Uwanja wa Mwadui Complex.
KMC iliyo nafasi ya sita na pointi 11 v Yanga, iliyo nafasi ya pili na pointi 16 saa 10:00 jioni, Uwanja wa CCM Kirumba.