Uncategorized

BM HATAHATI KUIKOSA YANGA NOVEMBA 7

admin October 27, 2020 9:47 am


KIUNGO wa Simba, Bernard Morrison kuna hatihati akaukosa mchezo wa dabi ya Kariakoo unaotarajiwa kuchezwa Novemba 7 dhidi ya watani zao wa jadi Yanga.


 Kwa mujibu wa Kanuni ya 39 (5)(5.2) mchezaji yeyote atayepigana au kupiga kabla ya mchezo au baada ya mchezo kumalizika basi atafungiwa michezo isiyopungua mitatu na faini isiyopungua sh. 500,00.


Pia Kanuni ya 39(6) mchezaji atayebainika kukutwa na makosa ya utovu wa nidhamu yanayojirudia au mara nyingi atafungiwa kucheza kati ya michezo 5 mpaka 10 na faini isiyopungua sh1m.


kutokana na kanuni hizo kama zitafuatwa kama zilivyo basi ni wazi kuwa mchezaji Morrison ataikosa Yanga kwa kuwa kanuni ya 35 inasema atafungiwa michezo 3 ambapo simba imebakisha michezo miwili ili kukutana na Yanga.


Kwenye mchezo wa Okotoba 26 uliochezwa Uwanja wa Uhuru kati ya Simba na Ruvu Shooting, Morrison alionekana akimpiga mchezaji wa Ruvu Shooting baada ya mchezo kusimama dakika ya 72 kutokana na kutokea kwa vurugu.


Vurugu hizo zilisababishwa na wachezaji wa Ruvu Shooting kugomea penalti waliyopewa Simba na ilipiga na John Bocco ambaye alikosa.


Kutokana na vurugu hizo mchezaji wa Ruvu Shooting, Shaaban Msala alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na mwamuzi wa kati ila BM hakuonyeshwa kwa kadi kwa kile ambacho ilionekana mwamuzi hajaona tukio hilo lililorushwa moja kwa moja na Azam Tv.

LIVERPOOL, MANCHESTER UNITED ZAIWINDA SAINI YA BERGMANN SARPONG: MUDA WANGU WA KUFUNGA BONGO UMEWADIA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply