Uncategorized

AZAM FC KUTESTI MITAMBO KUELEKEA MCHEZO WAO DHIDI YA KMC

admin November 14, 2020 11:47 am


 VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam FC leo Novemba 14 watakuwa na mchezo wa kutesti mitambo dhidi ya Mbeya Kwanza.


Azam kwenye ligi imecheza mechi 10 na imekusanya pointi 25 ikiwa nafasi ya kwanza chini ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba ambaye aliingia kwenye fainali na kocha bora wa mwezi Oktoba, Cedric Kaze wa Yanga.


Mchezo huu ni maalumu kwa ajili ya kujiweka sawa na mchezo wao wa ligi ujao ambao utakuwa ni dhidi ya KMC, wana Kino Boys unaotarajiwa kuchezwa Novemba 21.


Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa malengo makubwa ya timu hiyo ni kufanya vizuri kwenye mechi zote za ligi pamoja na mashindano mengine watakayoshiriki.

MARADONA ASHAURIWA KUACHA POMBE KOCHA BORA MWEZI OKTOBA, KAZE AWAPA TANO WACHEZAJI WAKE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply