Uncategorized

FIFA KUIPA LIVERPOOL MKWANJA MREFU SABABU YA GOMEZ

admin November 19, 2020 8:47 am


 SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (Fifa), linataka kuilipa Klabu ya Liverpool ambao ni mabingwa watetezi wa kombe la Ligi Kuu England kiasi cha pauni milioni 2 ambazo ni zaidi ya bilioni sita.


Fedha hizo ndefu ni kwa ajili ya malipo ya mshahara wa beki wao matata, Joe Gomez ambaye aliumia kwenye timu yake ya Taifa ya England ilipokuwa kwenye mazoezi na anaweza kukaa nje kwa muda mrefu.


Beki huyo ambaye aliumia goti analipwa pauni 80,000 kwa wiki akiwa ni miongoni mwa wachezaji wanaolipwa mkwanja mrefu ndani ya timu hiyo.


Fedha hizo zitalipwa na Fifa kwa kuwa wachezaji wa England wapo kwenye mradi wa msaada wa shirikisho kubwa la soka duniani lakini wakiwa na bima ambazo zinasimamiwa na Fifa. 

YANGA WAINGILIA KATI DILI LA MUKOKO KUIBUKIA SIMBA KILICHOMCHIMBISHA HITIMANA THIERY NDANI YA NAMUGO CHATAJWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply