Uncategorized

BEKI WA YANGA MWAMNYETO AMFUNIKA MAGUIRE WA MANCHESTER UNITED

admin November 25, 2020 9:47 am


 BEKI wa kati wa Klabu ya Yanga ya Bongo amemfunika jumlajumla beki wa kati ya Klabu ya Manchester United, Harry Maguire katika kuweka lango lake salama kwenye mechi za ligi ambazo wamezicheza.

Kwa Bongo, Yanga ikiwa imecheza jumla ya mechi 11, Mwamnyeto ameanza kikosi cha kwanza mechi 10 ambazo ni dakika 900 huku safu yake ya ulinzi ikiruhusu mabao manne. Maguire ameanza kikosi cha kwanza England mechi nane ambazo ni dakika 720 na timu yake imeruhusu mabao 13.



Mwamnyeto amekuwa na wastani wa kuokota bao moja kwenye nyavu kila baada ya dakika 225 licha ya kucheza mechi nyingi huku Maguire akiwa na wastani wa kuokota bao moja kila baada ya dakika 53.

Ingizo jipya la Yanga kutoka Coastal Union ndani ya dakika 900, ameonyeshwa kadi moja ya njano ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Namungo baada ya kumchezea faulo, Shiza Kichuya na kusababisha penalti moja huku Maguire ingizo jipya kutoka Leicester City ana jumla ya kadi mbili za njano.


JEMBE LINALOPIGIWA HESABU NA SIMBA LAINGIA ANGA ZA YANGA HIZI HAPA ZA LIGI KUU BARA LEO KUSAKA POINTI TATU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply