Uncategorized

SIMBA YAPEWA ULINZI WA KUTOSHA ABUJA, LEO KUANZA MAZOEZI RASMI

admin November 26, 2020 12:47 pm


 UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa wamepokelewa vizuri nchini Nigeria baada ya kuweka maandalizi ya awali na timu hiyo itakuwa kwenye ulinzi chini ya Serikali ili kuimarisha usalama kutokana na hali ya nchini Nigeria kutokuwa salama muda wote.


Kikosi hicho kiliwasili salama Nigeria jana, Novemba 25 ambapo mratibu wa Simba, Abas Ally alitangulia mapema kuweka mipango sawa.


Mratibu huyo amesema kuwa mazingira ya Nigeria ni mazuri na alipata ushirikiano mkubwa kutoka chama cha soka cha nchini Nigeria.


Aliongeza kuwa usalama wa hali ya Jos inaeleweka kuwa haipo sawa kwa wageni ambao wanafika ila kwa wenyeji wao wanaona kila kitu kinakwenda sawa lakini Simba imeweka wazi kwamba kwa mujibu wa wenyeji wao wamewaambia kwamba watawapa sapoti na kuwapa ulinzi wachezaji pamoja na benchi la ufundi.


Taarifa kutoka Simba zimeeleza kuwa kikosi leo kitaanza rasmi mazoezi Abuja, Nigeria kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Plateau FC ambao utapigwa siku ya jumapili, Novemba 29, 2020 kwenye uwanja wa New Jos uliopo mji wa Jos kuanzia saa 10:00 jioni (saa 12:00 jioni – Tanzania).

PRINCE DUBE KUPELEKWA AFRIKA KUSINI KWA AJILI YA MATIBABU ZAIDI YUSUPH MHILU: TUMEANZA KUJENGA HALI YA KUJIAMINI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply