Uncategorized

KMC YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA DODOMA JIJI

admin December 1, 2020 9:47 am


 UONGOZI wa KMC umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji unaotarajiwa kuchezwa Desemba 4, Uwanja wa Uhuru.


Ikiwa nafasi ya 7 baada ya kucheza mechi 11 inakutana na Dodoma Jiji iliyo nafasi ya 9 imecheza  mechi 12.


Kibindoni KMC imekusanya pointi 18 huku Dodoma Jiji ikiwa na pointi 16 zote zipo ndani ya 10 bora hivyo mchezo huo utakuwa na ushindani mkubwa.


Safu ya ushambuliaji ya KMC imefunga jumla ya mabao 15 huku ile ya Dodoma ikiwa imefunga mabao tisa.


Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa kila kitu kipo sawa na watapambana kupata pointi tatu mbele ya wapinzani wao.

KOCHA YANGA ATAJWA KUIBUKIA NDANI YA AZAM FC SIMBA YAPIGA HODI CAF

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply