Steve Barker Simba SC
Simba SC

Mtego wa Mechi 10: Steve Barker Atuma Onyo Zito Kuelekea Mchezo Dhidi ya JKT Tanzania!

Vardo November 20, 2026 8:31 pm

Mnyama Simba SC kesho anashuka dimbani akiwa na kibarua kimoja tu kichwani: kulinda heshima na kuendeleza wimbi la ushindi bila kupoteza mchezo wowote atakapowakaribisha maafande wa JKT Tanzania katika dimba la Ligi Kuu Tanzania Bara, Novemba 21, 2026.

Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Steve Barker, ameweka wazi kuwa hakuna lelemama, akisisitiza kuwa wachezaji wake wanapaswa kuingia uwanjani wakiwa na njaa ya ushindi na kujitoa kwa asilimia 100 ili kuhakikisha pointi tatu zinabaki nyumbani.

Akizungumza kuelekea mchezo huo wenye presha ya aina yake, Barker amekiri kuwa katika michezo miwili iliyopita kikosi chake hakikuonyesha makali yale yaliyozoeleka. Hata hivyo, amebainisha kuwa kipindi cha mapumziko ya ligi kimekuwa kama “dawa” iliyowarudisha mchezoni kwa kishindo.

“Mapumziko yametusaidia sana kukusanyika upya, kurejesha nguvu na kufanyia kazi mapungufu tuliyoyaona. Tunajua kila timu inayokutana na Simba sasa hivi inakuja na hasira ya kutaka kuwa ya kwanza kuvunja rekodi yetu,” amesema Barker.

Ili kuendeleza mfululizo wa ushindi wa mechi 10 mfululizo, kocha huyo raia wa Afrika Kusini amewataka nyota wake kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu na kulinda utambulisho wa soka la Simba.

“Imani yetu iko juu, na kujiamini kwetu kuko juu. Tuna wachezaji wenye uwezo wa kuamua mechi wakati wowote. Muhimu ni kuhakikisha tunatekeleza mipango yetu uwanjani kesho,” ameongeza kocha huyo kwa kujiamini.

Mbali na maandalizi ya uwanjani, Barker hakusita kuwapa maua yao mashabiki wa Msimbazi, akisema kelele na sapoti yao ndiyo injini inayowasukuma wachezaji kupambana hadi tone la mwisho. Ameahidi kuwa benchi la ufundi na wachezaji wanapambana kufa au kupona kuhakikisha mwaka huu wa kihistoria—ambao klabu inatimiza miaka 90—unapambwa na mataji na mafanikio makubwa.

Meridianbet Yatinga Mwananyamala, Yashusha Neema ya Vifaa vya Usafi Hospitali ya Kambangwa Miquissone Avunja Ukimya Baada ya Kutua Singida Black Stars: “Nilikumbuka Upendo na Vyakula vya Bongo”