Meridianbet Yatinga Mwananyamala, Yashusha Neema ya Vifaa vya Usafi Hospitali ya Kambangwa
Mazingira safi na salama ndiyo nguzo kuu ya afya bora kwa jamii yoyote. Kwa kulitambua hilo, kampuni ya Meridianbet imeamua kwenda hatua moja mbele zaidi ya burudani ya michezo na kubashiri, na safari hii imetua katika Hospitali ya Kambangwa, iliyopo Mwananyamala, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, kuacha alama ya tabasamu na usafi.
Kupitia programu yake endelevu ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), Meridianbet imekabidhi shehena ya vifaa muhimu vya usafi vyenye lengo la kuboresha mazingira ya utoaji huduma hospitalini hapo, na kufanya maeneo hayo kuwa rafiki zaidi kwa wagonjwa, wahudumu wa afya pamoja na wananchi wanaofika kupata matibabu.
Vifaa Vilivyokabidhiwa
Katika hafla hiyo fupi iliyojaa ushirikiano na furaha baina ya wawakilishi wa kampuni hiyo na uongozi wa hospitali, vifaa vifuatavyo vilikabidhiwa rasmi:
-
Buti imara za kazi (Boots) kwa ajili ya usalama wa wahudumu wa usafi.
-
Mifagio mikubwa ya kisasa (Big Mops) kurahisisha usafishaji wa wodi na korido.
-
Mapipa ya kuhifadhia taka (Dustbins) ili kuweka mazingira katika mpangilio nadhifu.
-
Sabuni maalumu za kuua vijidudu (Disinfectant Soap) kuhakikisha usalama wa kiafya dhidi ya maambukizi.
Kauli ya Meridianbet
Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo, mwakilishi kutoka Meridianbet, Nancy Ingram, alisisitiza kuwa maendeleo ya jamii ni sehemu isiyotenganishwa na utamaduni wa kampuni hiyo.
“Kusaidia jamii zenye uhitaji ni moja ya misingi mikuu inayotuongoza Meridianbet. Tunaamini kuwa tukishirikiana kwa karibu na wadau mbalimbali, tunaweza kupunguza changamoto zinazowakabili wananchi na kuleta mabadiliko chanya yanayoonekana katika maisha yao ya kila siku,” alisema Nancy Ingram.
Hatua hii ni mwendelezo wa falsafa ya Meridianbet ya kuhakikisha mafanikio yake yanarudi moja kwa moja kwa wananchi wanaowazunguka. Mbali na kugusa maisha ya jamii kwa vitendo, kampuni hiyo pia inaendelea kutoa burudani isiyo na kikomo kupitia michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa zenye odds kubwa na za ushindani.
Kwa yeyote anayetaka kuonja ladha ya ushindi huku akifurahia burudani ya kiwango cha juu, anaweza kujiunga leo kwa kutembelea tovuti rasmi ya Meridianbet au kupiga *149*10# ili kuanza safari yake ya ushindi.
