Uncategorized

KOCHA ARSENAL HANA HOFU YA KUCHIMBISHWA

admin December 1, 2020 12:47 pm

 


KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amesema hana hofu ya kufukuzwa licha ya kuwa timu yake imeendelea kuwa na matokeo mabaya.


 Wolves iliifunga Arsenal mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Emirates, juzi na hivyo kuongeza presha kubwa kwa Arteta kwa kuwa ni kipigo cha tatu mfululizo kwenye uwanja wa nyumbani.

 

Arteta amesema:-“Siku ambayo niliamua kuwa kocha nilijua kuwa ipo siku nitafukuzwa na ninaondoka kwenye klabu.


“Sijui kama siku hiyo ni lini, miezi sita au mwaka au miaka tangu niliposaini mkataba, hivyo sijawahi kuwa na hofu ya kufukuzwa.

 

“Ninachojali kwa sasa ni kufanya wachezaji wangu wacheze vizuri, kufanya mazuri kwa timu ili kupata matokeo mazuri.

 

“Ninajua kwa taaluma hii ipo siku nitafukuzwa au nitaondoka mwenyewe, sijui lini itakuwa hivyo,” amesema kocha huyo.

SIMBA YAPIGA HODI CAF M-Bet YAZINDUA KAMPENI YA ZAMU YAKO, YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI 94

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply