Uncategorized

NYOTA WANNE WA YANGA WAWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA NOVEMBA

admin December 1, 2020 2:47 pm


 NYOTA wanne wa Klabu ya Yanga wanapambania tuzo ya mchezaji bora kwa mwezi Novemba ambao umekamilika jana.


Ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 31 baada ya kucheza mechi 13.


Wachezaji hao wanaowania tuzo hiyo ni pamoja na kipa namba moja Metacha Mnata ambaye amecheza jumla ya mechi 12 kati ya 13 na beki chipukizi, Bakari Mwamnyeto.

Pia yupo kiraka Deus Kaseke ambaye amefunga jumla ya mabao mawili kwenye mechi mbili mfululizo ilikuwa mbele ya Azam FC na JKT Tanzania.


Mshambuliaji mwenye spidi ila hana bahati ya kufunga naye yumo kwenye orodha hiyo ambaye ni Yacouba Songne mwenye bao moja na pasi mbili za mabao.


Ili kumpigia kura mchezaji unayempenda, Yanga wameweka utaratibu kwamba unampigia kura kupitia akaunti yao ya Twitter,’yangasc1935′.

PIALALI ALIYEMKALISHA TINAMPAY, MTANGO WATOA NENO LA SHUKRANI KUNA JEMBE LA MABAO LINAKUJA YANGA,SVEN ANA JAMBO LAKE,KESHO NDANI YA CHAMPIONI JUMATANO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply