Uncategorized

BREAKING:LWANGA ASAINI DILI JIPYA SIMBA

admin December 2, 2020 10:47 am

Kiungo mkabaji (defensive midfielder) wa kimataifa wa timu ya Taifa ya Uganda ambaye amewahi kuzichezea timu za Express FC, SCV Kampala, Vipers FC na Tanta FC, Taddeo Lwanga amesaini dili la miaka miwili kuitumikia Klabu ya Simba.


Nyota huyo alikuwa kwenye rada za mabosi hao kwa muda mrefu baada ya kiungo wao Gerson Fraga kupata majeraha ambayo yatamuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Fraga aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United na nafasi yake ilichukuliwa na Said Ndemla ambaye ni mzawa.


 Usajili wa Lwanga unatokana na Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) kutoa nafasi za wawakilishi wa mashindano ya kimataifa kusajili wachezaji 10 ili kuongeza nguvu katika mashindano hayo. 

MABADILIKO NDANI YA YANGA MCHAKATO WAFIKA PATAMU KATWILA: DIRISHA DOGO TUTAFANYA USAJILI UTAKAOTUBEBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply