Uncategorized

MASHABIKI WA YANGA WAPIGWA ‘PINI’ KIMTINDO NA SIMBA

admin December 3, 2020 11:47 am


 UONGOZI wa Simba umesema kuwa unawataka mashabiki wote watakaoingia Uwanja wa Mkapa kuishuhudia timu hiyo ikimenyana na Plateau United wavae jezi za Simba na kugoma kuwaruhusu mashabiki wengine tofauti na timu hiyo.


Mpango huo ni maalumu kwa ajili ya kuwapiga pini wale mashabiki ambao huvaa jezi za njano kila Simba ikiwa inacheza michezo ya kitaifa na kimataifa ambao wanatajwa kuwa ni wa Yanga ambao huwazomea pale wanapopata matokeo mabaya.


Haji Manara Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa hakutakuwa na ruhusa kwa mashabiki wa kuwazomea kuingia uwanjani kwa kuwa wamepaga mpango maalumu utakawafanya wawapate wale ambao wanawahitaji.


Mchezo huo utakuwa ni wa marudio unatarajiwa kuchezwa Desemba 5, Uwanja wa Mkapa baada ya ule wa awali uliochezwa Uwanja wa New Jos Nigeria, Novemba 29 Simba kushinda bao 1-0 ikiwa ugenini.


Manara amesema:”Hatutawaruhusu mashabiki wa aina nyingine tofauti na Simba kuingia uwanjani, tunataka mashabiki 30.000 tulioruhusiwa na CAF kuingia uwanjani wote wawe wa Simba,” .

SIMBA YAINGIA ANGA ZA KIPA MRUNDI, ALIWABANIA YANGA KISSU ATAFUTIWA MBADALA WAKE NDANI YA AZAM FC

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply