Uncategorized

SIMBA YAFAFANUA SABABU YA KUWATAKA MASHABIKI WAKE WANUNUE TIKETI KWA WINGI

admin December 4, 2020 2:47 pm

UONGOZI wa Simba umesema kuwa nafasi walizopewa kwa ajili ya mchezo wa kesho wa marudio wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Plateau United hazitoshi jambo ambalo lilimfanya aseme kuwa wanampango wa kuwaruhusu mashabiki wa Simba wajitokeze kushangilia kwa wingi.


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wengi wamekuwa wakitafsiri vibaya jambo hilo kwa kuwa hawakuelewa maana yake aliposema kuwa wanahitaji mashabiki wa Simba wajitokeze kwa wingi kuishabikia timu hiyo.

Manara amesema:”Nafasi 30,000 hazitutoshi Simba kwa kuwa tuko wengi, ndio maana nilitaka waje Simba wengi kushangilia. Nafikiri kuna watu hawakunielewa makusudi au bahati mbaya.


“Ndio maana nimejitokeza na kusema tuwafundishe Yanga ustaarabu, kama ikitokea shabiki wetu ameingia tusilipe kisasi, lazima tuendeleze ule utamaduni wetu wa kujali na upendo kwa kila shabiki bila kubagua.

“Mashabiki wa Simba wamepigwa dhidi ya Azam, wamepigwa dhidi ya Mtibwa na wako ambao hawakusema. Sasa mashabiki wa Simba, wawafundishe hawa kwa ustaarabu,” amesema.

MTANZANIA ASEPA NA TUNZO ULAYA BAADA YA KUTUPIA MABAO MANNE KMC YATEMBEZA PIRA SPANA YASEPA NA POINTI TATU MBELE YA DODOMA JIJI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply