Uncategorized

SIMBA KUCHEZESHWA PIRA SPANA LEO KWA MKAPA

admin December 16, 2020 12:47 pm


 UONGOZI wa KMC umesema kuwa utacheza pira spana mbele ya Simba na kusepa na pointi tatu muhimu ndani ya Uwanja.


Simba itawakaribisa KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkapa huku kila timu ikitamba kusepa na pointi tatu muhimu.


Mchezo wao wa mwisho msimu uliopita kukutana uwanjani, Simba ilishinda mabao 2-0 hivyo leo KMC itaingia uwanjani ikiwa na hesabu za kulipa kisasi.


Pia KMC bado ina maumivu ya kuyeyusha pointi tatu dhidi ya Mtibwa Sugar baada ya kufungwa bao 1-0 huku ikitambua kwamba inakutana na Simba ambayo imetoka kushinda bao 1-0 dhidi ya Mbeya City.

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema””Ipo wazi na tunatambua kwamba tunakutana na Simba ikiwa imetoka kushinda mbele ya Mbeya City huko Mbeya.


“Walishinda mbele ya Mbeya City sasa wanakutana na Kino Boys, tutacheza pira spana, pira kodi, pira mapato lengo ikiwa ni kupata pointi tatu.


“Mashabiki wajitokeze kwa wingu kutupa sapoti ili kuona namna gani tunaondoka na pointi tatu muhimu,” .


KMC ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 21 inakutana na Simba iliyo nafasi ya pili na pointi 29.

NYOTA MPYA YANGA NTIBANZOKIZA ATOA KAULI YA MATUMAINI NYOTA MKENYA WA YANGA SAFARI IMEWADIA, KUMPISHA KIUNGO MRUNDI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply