Uncategorized

LAMPARD ASHANGAZWA NA SILVA

admin December 22, 2020 7:47 am


 FRANK Lampard, Kocha Mkuu wa Chelsea amesema kuwa uwezo wa nyota wake Thiago Silva wakati wakishinda mabao 3-0 dhidi ya West Ham United ulimshangaza kwa kiasi kikubwa.

Silva alianza kupachika bao la kwanza dakika ya 10 huku yale mawili yakipachikwa na Tammy Abraham dakika ya 78 na 80 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England, uliochezwa Uwanja wa  Stamford Bridge. 

Ushindi huo unaifanya Chelsea kufikisha jumla ya pointi 25 ikiwa nafasi ya 5 na West Ham United ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi 21 zote zimecheza jumla ya mechi 14.

Lampard amesema kuwa hakutarajia kuona kiwango bora kwa nyota huyo jambo analoamini kwamba atakuwa mchezaji mkubwa wakati ujao.

“Nimeshangazwa na uwezo wake na ninajivunia uwepo wake, ninajua kwamba wakati ujao atakuja kuwa bora na mchezaji mkubwa,” .

WAWILI WA SIMBA HATIHATI KUIVAA FC PLATINUM LAMPARD ASHANGAZWA NA SILVA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply