Uncategorized

WAWILI WA SIMBA HATIHATI KUIVAA FC PLATINUM

admin December 22, 2020 6:47 am



KUNA hatihati ya nyota wawili wa kikosi cha Simba, kipa namba moja, Aishi Manula na mshambulaiji wao John Bocco wakaukosa mchezo wa kesho,  Desemba 23.

Simba itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao unatarajiwa kuchezwa kesho Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe. 

Mchezo huo utachezwa majira ya saa 9:00 alasiri kwa saa za Zimbabwe huku kwa Tanzania ikiwa ni saa 10:00 jioni.

Nyota hao wawili walipata maumivu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC ambapo Simba ilishinda bao 1-0 lilipachikwa kimiani na Meddie Kagere ambaye ametupia jumla ya mabao matano kwa msimu wa 2020/21.

Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa wachezaji hao watafanyiwa tathimini kwenye mazoezi ya leo ili kujua uwezekano wao wa kuweza kucheza kesho.


Manula alitumia jumla ya dakika 180 kwenye mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali ilikuwa mbele ya Plateau United ambapo ugenini, nchini Nigeria Simba ilishinda bao 1-0 na mchezo wa marudio uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Simba ililinda ushindi wake.

BEKI SIMBA KUIBUKIA UTURUKI LAMPARD ASHANGAZWA NA SILVA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply