Uncategorized

KOCHA WA ZAMANI WA SPURS AKUBALI KUTUA PSG

admin December 25, 2020 10:47 am

 


MAURICIO Pochettino Kocha wa zamani wa Klabu ya Spurs amekubali kubeba mikoba ya Thomas Tuchel aliyefukuzwa ndani ya Klabu ya PSG.

Tuchel alifutwa kazi jana Desemba 24 kutokana na mwendo mbovu wa timu hiyo ikiwa ipo nafasi ya tatu ndani ya Ligue 1.

Pochettino amefikia mazungumzo mazuri na PSG kuhusu kubeba mikoba ya Tuchel huku kukiwa na uwezekano mkubwa kwa raia huyo wa Argentina kuanza kazi hivi karibuni.

Hajawa na timu baada ya kufutwa kazi ndani ya Spurs Novemba 2019 ambapo alikuwa anatajwa pia kuibukia ndani ya Manchester United.

Taarifa zinaeleza kuwa maneno ya Tuchel kwamba timu hiyo inaendeshwa kwa siasa yanatajwa pia kumpoza jambo lililosababisha mabosi kumfuta kazi jumlajumla.

CRISTIANO RONALDO ATUMA SALAMU ZA CHRISTMAS SIMBA KUREJEA BONGO KUIVUTIA KASI MAJIMAJI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply