Uncategorized

ISHU YA NYOTA WA YANGA KUIBUKIA IHEFU YABUMA

admin January 2, 2021 6:47 am


 UONGOZI wa Yanga kupitia kamati yake ya usajili, imewachinjia baharini mabosi wa Ihefu FC, kufuatia barua yao ya kumtaka mshambuliaji wao Waziri Junior, akajiunge nao kwa mkopo.

 

Takribani mwezi mmoja sasa Ihefu iliandika barua yake kwa uongozi wa Yanga, ukimuomba Waziri ajiunge na kikosi chao baada ya kusikia wanataka kumtoa kwa mkopo.


 Kocha Mkuu wa Ihefu, Zubeir Katwila ameweka wazi kuwa, pamoja na kuendelea kuaminishwa na uongozi wa Yanga kuwa atapewa saini ya Waziri, amepata habari za ndani kuwa mchezaji huyo huenda akapelekwa Coastal Union ya Tanga.

 

“Nimesikia kuna uwezekano wa kumkosa Waziri, ambaye tuliwaomba Yanga watupatie kwa mkopo tena mapema kabisa, nilimtegemea sana Waziri kuja kutusaidia ila kama kweli wameamua kutotupatia siyo mbaya.


“Kwa sasa tutajitahidi kuwatumia washambuliaji ambao tumewapata kipindi hiki lengo likiwa ni moja kupata matokeo chanya” amesema Katwila.

BABAYE KAGERE NI MTANZANIA, NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI JONAS MKUDE AWAPOTEZA WOTE NDANI YA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply