Uncategorized

SPURS WAENDELEZA MAKALI,KANE NA SON NI HABARI NYINGINE

admin January 3, 2021 5:47 am


 HARRY Kane nyota wa Klabu ya Tottenham Spurs inayonolewa na Kocha Mkuu, Jose Mourinho amesema kuwa maisha yao ndani ya timu hiyo ni ya furaha kubwa jambo linalomfanya azidi kuwa na furaha kila anapofunga.

Son Heung-min na Kane wamekuwa na ushirikiano mkubwa ndani ya uwanja ambapo wamekuwa ni tegemeo kwenye kikosi hicho kwa pamoja Jumamosi walifunga mabao wakati timu yao ikishinda mabao 3-0 dhidi ya Leeds United.

Leeds United haikuwa na bahati mbele ya Tottenham Hotspur baada ya kuokota mabao matatu kambani kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Tottenham Hotspur.


Mabao ya Spurs yalifungwa na Harry Kane dakika ya 29 kwa mkwaju wa penalti, Son Heung-min dakika ya 43 na msumari wa mwisho ulikomelewa na Toby Alderweireld dakika ya 50.

Matt Doherty dakika ya 90+2 alionyeshwa kadi nyekundu. Matokeo hayo yanaifanya Spurs kufikisha jumla ya pointi 29 ikiwa nafasi ya tatu na Leeds United nafasi ya 12 na pointi 23.


Kane amesema:”Ikitokea nikafunga mimi ni sawa hata akifunga mwingine sina tatizo ila kikubwa tunahitaji ushindi ndani ya timu hakuna jambo jingine,”.
JEMBE JIPYA AZAM FC LAPANIA KUTUPIA MABAO ZAIDI YA 15 TAULO LA JUMA KASEJA LAZUA ‘TIMBWILI’ MBEYA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply