Uncategorized

NYOTA TISA WA YANGA ‘OUT’ KOMBE LA MAPINDUZI

admin January 4, 2021 9:47 am

 


NYOTA tisa wa kikosi cha kwanza ndani ya Yanga wanatajiwa kukosa michuano ya Kombe la Mapinduzi ambalo linatarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho, Januari 5 .


Bingwa mtetezi wa taji hilo la heshima litakalofanyika visiwani Zanzibar ni Mtibwa Sugar ambaye atafungua pazi hilo kesho, Januari 5 kwa kuanza kumenyana na Chipukizi saa 10:15 jioni.


Mchezo wa kwanza kwa Yanga ambayo itasepa leo ni dhidi ya Jamhuri utakaochezwa saa 8:15 Uwanja wa Amaan.


Nyota hao ni Yassin Mustapha, Bakari Mwamnyeto, Farid Mussa, Feisal Salum, Ditram Nchimbi na Deus Kaseke ambao wapo kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania inayojiandaa na michuano ya Chan 2021.

Balama Mapinduzi yeye ni mgonjwa na kiungo Carlos Carlinhos huku Yacouba Songne akiwa amepewa mapumziko ya wiki moja kutibu majeraha yake ya mbavu. 

MTAMBO WA MABAO YANGA NJE WIKI MOJA, KUKOSA MECHI ZA MAPINDUZI SIMBA YAFUNGUKIA ISHU YA MKUDE KUFUKUZWA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply