Uncategorized

KMC WALITAKA TAJI LA KOMBE LA SHIRIKISHO

admin January 6, 2021 5:47 am

 


UONGOZI wa KMC umesema kuwa unahitaji kutwaa Kombe la Shirikisho hivyo wapinzani wao wajipange kupokea kichapo watakapokutana uwanjani.


Jana, Januari 5 ilishinda bao 1-0 dhidi ya Lipuli FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru. 

Bao pekee la ushindi kwa KMC lilifungwa na Cliff Buyoya ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo. 


Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa wanahitaji kutwaa Kombe la Shirikisho lililo mikononi mwa Simba.


“Tumejipanga baada ya kupita hatua hii tunakwenda kufanya vizuri mechi zinazofuata na tunahitaji kutwaa Kombe la Shirikisho hatuna mashaka na uwezo wetu,” .

SIMBA: KAMA MWARABU ALIKUFA KWA MKAPA FC PLATINUM HAWATOKI MKWASA WA RUVU SHOOTING NI HABARI NYINGINE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply