Uncategorized

JEMBE JIPYA AZAM FC KUANZA KUKINUKISHA LEO

admin January 7, 2021 10:47 am


 INGIZO jipya ndani ya kikosi Cha Azam FC Mpiana Monzinzi anayefundishwa na Kocha Mkuu, George Lwandamina anatarajiwa kuanza leo kutumika ndani ya timu yake mpya.


Leo Januari 7, Azam FC inakazi ya kusaka ushindi mbele ya Mlandege utakaochezwa Uwanja wa Amaan, majira ya saa 8:15 usiku.

Mshambuliaji huyo amesaini dili jipya kwenye usajili wa dirisha dogo lililofunguliwa Desemba 16 na linatarajiwa kufungwa Januari 15

Amechukua mikoba ya mshambuliaji Thiery Akono ambaye amesepa zake na kuelekea kucheza soka a kulipwa nchini Malysia.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema:-“ITC ya Mpiana Monzinzi imeshafika na kuanzia sasa yuko tayari kuitumikia Azam FC.

“Matumaini yetu ni kuona kwamba anafanya vizuri kwa kuwa ameshaanza kuzoeana na wachezaji wenzake pamoja na kupewa maelekezo kutoka kwa benchi la ufundi,” .


Nyota huyo raia wa Congo ambaye alikuwa anacheza ndani ya FC Lupopo amesema:”Ninafurahi kuwa ndani ya Azam FC, furaha yangu ipo kwenye kufunga na nina amini kwamba itakuwa hivyo,” .


Mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi ni Mtibwa Sugar, mchezo wao wa ufunguzi walishinda bao 1-0 dhidi ya Chipukizi.

DODOMA JIJI BANA, WATEMBEZA 5G, WAOMBA RADHI KWA MASHABIKI RASTA STARS ANAYEWINDWA NA YANGA AKUBALI KUSAINI SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply