Uncategorized

AZAM FC KUPIGA KAMBI ZANZIBAR SIKU 10

admin January 13, 2021 3:47 pm

 


BAADA ya Mabingwa mara tano wa Kombe la Mapinduzi, Azam FC kutolewa na Yanga hatua ya nusu fainali kwa kufungwa penalti 5-4 kitabaki Visiwani Zanzibar kwa kambi ya siku 10.

Dakika 90 za nusu fainali ya kwanza ilikamilika kwa Azam FC kufungana bao 1-1 dhidi ya Yanga na kupelekea kufika hatua ya kupigiana matuta.

Hatua hiyo iliwafungashia virago mazima Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina raia wa Zambia.

Azam FC kwa sasa imeanza maandalizi ya mechi zake za Ligi Kuu Bara ikiwa ni mzunguko wa pili.

Mchezo wake unaofuata ni Januari 16 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Coastal Union ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 20 baada ya kucheza mechi 18 inakutana na Azam FC iliyo nafasi ya tatu na pointi zake 32. 

KIKOSI CHA YANGA KINACHOTARAJIWA KUANZA LEO DHIDI YA SIMBA, KOMBE LA MAPINDUZI KIKOSI CHA SIMBA KINACHOTARAJIWA KUANZA LEO DHIDI YA YANGA, KOMBE LA MAPINDUZI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply