Taifa Stars

KOCHA STARS:BADO TUNA NAFASI YA KUFANYA VIZURI CHAN

admin January 20, 2021 11:47 am


 SELEMAN Matola, kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa vijana walicheza vizuri ila makosa yaliwafanya washindwe kupata matokeo ndani ya uwanja.

Matola amesema kuwa nafasi ya kufanya vizuri ipo kwa kuwa wana mechi mbili mkononi za kucheza kwenye mashindano hayo ambayo yanahusisha wachezaji wa ndani.

Jana, Januari 19 Stars ilifungua pazia ndani ya Chan kwa kufungwa mabao 2-0 ambapo moja ilifungwa kwa mkwaju wa penalti na moja kwa shuti kali la nje ya 18.

Matola amesema kuwa wachezaji kipindi cha kwanza walifanya kazi kubwa ya kusaka ushindi ila mambo yalikua magumu kwao na kipindi cha pili makosa waliyofanya yaliwagharimu.

“Wachezaji walicheza vizuri kipindi cha kwanza ila kipindi cha pili makosa ambayo walifanya yameweza kuleta mabao ya kufungwa.

“Naona kwamba bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi zetu ambazo zimebaki kikubwa ni kuendelea kutoa sapoti na kila kitakuwa sawa,” amesema.

Mchezo unaofuata kwa Stars nchini Cameroon ni dhidi ya Namibia itakuwa ni Jumamosi, Januari 23.

CARLINHOS AREJESHWA YANGA, KUANZA MAZOEZI CRYSTAL PALACE KUTHIBITISHA KUPATA SAINI YA JEAN

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply