Simba SC

JONAS MKUDE ATOZWA FAINI YA SH. MIL 2, ATAKIWA KUREJEA KAMBINI

admin January 23, 2021 6:16 pm


Kamati ya Nidhamu ya Klabu ya Simba chini ya Mwenyeki wake Suleiman Kova imetangaza hukumu ya kiungo wa klabu hiyo, Jonas Mkude ambaye alisimamishwa na uongozi kwa makosa ya utovu wa nidhamu.

Kwa mujibu wa  Kova, haya ndiyo makosa aliyokuwa akituhumiwa kuyafanya, pamoja na hukumu zake.

KOSA LA KWANZA: Kutohudhuria semina elekezi iliyohusisha wachezaji, benchi la ufundi na viongozi. Adhabu yake ni faini ya shilingi milioni moja (1,000,000).

KOSA LA PILI: Kuchelewa kuingia kambini wakati timu ilipokuwa ikijiandaa na mchezo dhidi ya Coastal Union. Adhabu aliyopewa ni karipio kali na faini ya shilingi milioni moja (1,000,000) na kuwekwa katika kipindi cha uangaizi cha miezi sita.

KOSA LA TATU: Kutoripoti kambini siku ya 26/11/2020 bila ruhusa. Katika tuhuma hizi, kamati haikumkuta na hatia baada ya kamati kutothibitisha pasipo shaka shitaka hilo.

MAAGIZO
Kamati imemtaka Mkude kurejea kambini mara moja kuendelea na mazoezi na asipofanya hivyo atakuwa amefanya tena kosa la utovu wa nidhamu.

Faini aliyotozwa anatakiwa kuilipa ndanI ya mwezi mmoja.

Kamati imemtaka Mkude kuomba radhi kwa maandishi ndani ya saa 24
BEKI SIMBA ATISHWA NA PACHA YA SAIDO, FISTON YANGA HILI HAPA JESHI LA STARS DHIDI YA NAMIBIA LEO USIKU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply