Ligi Kuu

WANA KINO BOY WAENDELEA KUJIWEKA SAWA KWA AJILI YA LIGI KUU BARA

admin January 25, 2021 4:47 am

 KIKOSI cha KMC , Wana Kino Boys leo kinatarajiwa kuendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiweka sawa na michezo yao ya Ligi Kuu Bara wa mzunguko wa pili unaotarajiwa kuanza Februari 13.

Leo kitakuwa Uwanja wa White Sands majira ya saa 9:00 alasiri kuendelea kujiweka sawa kwa ajili ya mechi zao zijazo.

KMC kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ipo nafasi ya 7 baada ya kucheza mechi 17. Imekusanya pointi 22.

Kinara wa Ligi Kuu Bara ni Yanga mwenye pointi 44 baada ya kucheza jumla ya mechi 18 huku anayeburuza mkia ni Ihefu mwenye pointi 13 baada ya mechi 18.

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa mipango ya timu hiyo ni kufanya vizuri mzunguko wa pili.

“Timu ipo vizuri na tumeanza maandalizi kwa ajili ya mzunguko wa pili hivyo matumaini yetu tutakuwa katika kasi nzuri ambayo tulianza nayo awali.

“Kikubwa mashabiki wazidi kutupa sapoti katika kile ninachokifanya kila kitu kitakuwa sawa,”.

AZAM FC KUREJEA KAMBINI LEO RASMI KOCHA MPYA SIMBA APANGA KUISHUSHA YANGA KILELENI MAPEMA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply