DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, raia wa Ufaransa ameanza kazi rasmi ya kukinoa kikosi hicho akiwa na mitambo iliyotupia jumla ya mabao 17 ndani ya Ligi Kuu Bara.
Zama zile za Sven Vandenbroeck, Simba baada ya kucheza jumla ya mechi 15 ilitupia jumla ya mabao 37 huku kinara wa utupiaji ni John Bocco mwenye mabao nane na ana pasi mbili za mabao.
Mbali na kuanza kazi na mabao hayo 17, Januari 24 mara baada ya kumaliza kusaini dili la miaka miwili ndani ya Simba pia nyota hao wametengeneza jumla ya nafasi 17 ambazo zilileta mabao na kufanya wahusike kwenye mabao 34.
Nyota hao ni:-Bernard Morrison yeye ametupia bao moja na ana pasi mbili za mabao, Rally Bwalya pasi moja ya bao, Clatous Chama mwenye mabao sita na pasi nane za mabao,Ibrahim Ajibu sawa na Mohamed Hussein kila mmoja ana bao moja na pasi moja ya bao, Mzamiru Yassin mabao mawili na pasi moja ya bao Hassan Dilunga mabao mawili na pasi tatu za mabao na Chris Mugalu mabao manne.
Thadeo Lwanga, Perfect Chikwende na Junior Lokosa hawa ni wapya ndani ya kikosi wanaungana na Miraj Athuman, David Kameta, Kened Juma Gadiel Michael, Ally Salim, Francis Kahata na Beno Kakolanya ambao bado wanapambana kuweka rekodi ndani ya Simba.
Mchezo wake wa kwanza kukaa benchi ilikuwa jana Januari 27 kwenye mchezo wa Simba Super Cup ambapo ilikuwa ni mbele ya Al Hilal.
Kwenye mchezo huo Simba ilishinda mabao 4-1 Uwanja wa Mkapa huku wafungaji wa mwanzo chini ya Gomes ni Rarry Bwalya ambaye alikuwa nyota wa mchezo huo na alisepa na zawadi ya laki tano.
Perfect Chikwende ambaye ilikuwa ni mchezo wake wa kwanza ndani ya ardhi ya Bongo akiwa na Simba baada ya kujiunga na timu hiyo akitokea Klabu ya FC Platinum pamoja na Morrison ambaye alitupia mabao mawili.
Nyota wawili walitengeneza nafasi za mabao ni Mugalu na Miraji Uwanja wa Mkapa.