Yanga SC

MTAMBO WA MABAO WA YANGA KUTUA LEO

admin January 28, 2021 8:47 am


 MTAMBO mpya wa mabao ndani ya Klabu ya Yanga, Fiston Abdoul unatarajiwa kutua leo kwenye ardhi ya Bongo kwa ajili ya kujiunga na vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga akitokea nchini Burundi.

Nyota huyo ambaye amejenga ushkaji mkubwa na kucheka na nyavu amesaini dili la miezi sita lenye kipengele cha kuongeza mkataba ikiwa atafanya vizuri ndani ya muda ambao atahudumu ndani ya kikosi hicho.

Ana rekodi ya kufanya vizuri pia kwenye michuano ya Afcon ambapo alikuwa ni miongoni mwa washambuliaji wenye mabao mengi ambapo alifunga jumla ya mabao sita jambo ambalo linampandisha chati nyota huyo.

Uongozi wa Yanga umeeleza kuwa nyota huyo anatarajiwa kutua leo rasmi kujiunga na timu hiyo ambayo inanolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze.

Fiston amesema kuwa anakuja Bongo akiwa anaitambua vema ligi pamoja na ushindani ulivyo hivyo hana tabu na kile ambacho atakuja kukifanya.

Kwenye msimamo yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 44 baada ya kucheza jumla ya mechi 18.

AZAM FC:DUBE AMEPONA KWA SASA VIBALI VYA NYOTA MPYA WA SIMBA CHIKWENDE BADO, LOKOSA SAFI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply