Azam FC

AZAM FC YAINYOOSHA KMC MABAO MATATU AZAM COMPLEX

admin January 31, 2021 2:47 am

 VIVIER Bahati,  kocha msaidizi wa Klabu ya Azam FC amesema kuwa bado vijana wake wanazidi kuimarika jambo ambalo limewafanya waibuke na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya KMC.

Azam FC iliibuka na ushindi huo kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa jana Januari 29, Uwanja wa Azam Complex. 

Mabao ya Azam FC mawili yalifungwa na Prince Dube na moja lilipachikwa na Mudhathir Yahya huku lile la KMC likipachikwa na Lusajo Mwaikenda aliyepachika bao hilo kwa penalti.

Bahati amesema:”Ulikuwa ni mchezo mzuri na kila mchezaji alikuwa kwenye wakati mzuri jambo ambalo limetufanya tuwe katika wakati mzuri kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara ambazo zinakuja,”.

JEMBE JIPYA YANGA LAANZA KAZI MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply