Steve Barker Simba SC
Simba SC

Steve Barker Kutaka Mwisho Mtamu Singida: “Tupo Tayari Kwa Pointi Tatu!”

Vardo August 21, 2026 3:16 pm

KOCHA Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, ameweka wazi kuwa kikosi chake kipo kwenye hali nzuri ya kimwili na kisaikolojia kuelekea pambano la Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida Black Stars kwenye Uwanja wa Airtel, Singida.

Mchezo huo unakuwa wa tatu kwa Wekundu wa Msimbazi ndani ya wiki moja tangu kufunguliwa kwa msimu mpya. Simba inaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar na ushindi wa 2-1 dhidi ya Pamba FC.

Barker ameeleza kuwa licha ya ratiba kuwa na msongamano mkubwa pamoja na safari ndefu ya kuelekea Singida, wachezaji wake wamepata muda wa kutosha wa mapumziko na wako tayari kupambana.

β€œNi mchezo wetu wa tatu ndani ya wiki hii. Baada ya safari ndefu ya jana, wachezaji wamepumzika vizuri na kurejea kwenye hali yao ya kawaida. Morali ni ya juu na wote wana afya njema,” alisema Barker.

Kocha huyo amesisitiza kuwa lengo kuu la Simba katika mchezo huo wa ugenini ni kuondoka na pointi zote tatu ili kumaliza ratiba hiyo ngumu kwa matokeo chanya.

β€œTumeanza msimu vizuri na ni muhimu kuendeleza kasi hii. Tunataka kumaliza wiki hii kwa ushindi ili kujenga mwendelezo mzuri wa matokeo katika kampeni yetu ya ubingwa,” aliongeza.

Tabitha Chawinga: Temwa Anastahili Ballon d’Or 2026 Ali Kamwe Afichua Sababu Gomez, Aziz Ki Kuchelewa Yanga SC