Ligi Kuu

MTIBWA SUGAR YAANZA KUPIGIA HESABU MZUNGUKO WA PILI

admin January 31, 2021 4:47 am


 HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa tayari wachezaji wa timu hiyo wamerudi kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili.

Mtibwa Sugar walivunja kambi baada ya kuvuliwa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi na Simba visiwani Zanzibar.

Akizungumza na Saleh Jembe, Hitimana ambaye aliibuka ndani ya Mtibwa Sugar baada ya kufutwa kazi ndani ya Klabu ya Namungo FC amesema kuwa tayari maandalizi yameanza.

“Taratibu kwa sasa tumeanza maandalizi kwa ajili ya mechi zetu za Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili na nina amini kwamba tutakuwa imara.

“Ipo wazi kwamba mzunguko wa pili utakuwa na ushindani mkubwa ila mashabiki wasiwe na presha wazidi kutupa sapoti nina amini kwamba tutafanya vizuri na kila kitu kitakuwa sawa,” .

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 11 baada ya kucheza jumla ya mechi 18 na kibindoni ina pointi 22.

RASHFORD:NINAJUA KWAMBA MIMI NI MWEUSI, WANAONIBAGUA SITAWAJIBU MWISHO WA UBISHI GLOBAL FC V DStv LEO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply