Home Simba SC BAADA YA SUPER CUP…BARBARA AFUNGUKA MIKAKATI HII MIKUBWA YA KUIPAISHA SIMBA KIMATAIFA..!!

BAADA YA SUPER CUP…BARBARA AFUNGUKA MIKAKATI HII MIKUBWA YA KUIPAISHA SIMBA KIMATAIFA..!!


OFISA Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara amesema ana malengo matatu makubwa mbele yake, ambayo anatakiwa kuyatimiza msimu huu.

Barbara alisema malengo hayo ni kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu na bado wana mechi zaidi ya 20 hadi kumaliza msimu, lakini la pili ni kuifikisha timu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambalo tayari amelifikia.

“Jambo la tatu ambalo nimewekewa na natakiwa kulifikia ni kutetea ubingwa wa Kombe la Shirikisho (ASFC), ambalo tupo katika hatua ya pili na kwa jinsi ya kikosi chetu kilivyo bora hilo linawezekana,” alisema Barbara.

Katika hatua nyingine, Barbara alisema misimu miwili iliyopita katika Ligi ya Mabingwa Afrika hawakufanya vizuri kwenye mechi za ugenini, lakini msimu huu mambo yatakuwa tofauti.

Alisema katika kuhakikisha ugenini wanakuwa na matokeo mazuri pia wamesajili wachezaji wenye uwezo wa kwenda kuipigania timu huko tofauti na misimu miwili iliyopita kikosi hakifanani na sasa.

“Kama uongozi tumeongeza hali ya kujiamini kwa wachezaji ambayo haikuwepo pindi tulipokuwa tunakwenda kucheza ugenini, lakini tumeajili wataalamu kama Culvin Mavunga (Video analystis) ili kuipa nguvu benchi la ufundi kwenye mechi za mashindano yote.

“Ukiangalia tumeboresha benchi la ufundi kwa kuwaleta watu wenye uwezo kama kocha mkuu, Didier Gomes, kocha wa makipa, mtaalamu wa mazoezi ya viungo ambaye anayetumia kifaa chenye (GPRS).

“Sayansi ambayo tunaitumia katika timu kwa wakati huu ni kubwa mno na teknolojia tunayoitumia inatusaidia sana na kuna baadhi ya mambo mengine ya msingi na mikakati ya kuona tunafanya vizuri zaidi katika timu msimu huu siwezi kuiweka wazi,” alisema Barbara.

SOMA NA HII  SIMBA YALITAKA KOMBE LAKE, YAPANIA KUSHINDA MBELE YA AZAM FC