Home Yanga SC YANGA WATAJA SABABU YA KUSAJILI VIJANA,KAZE ATOA NENO

YANGA WATAJA SABABU YA KUSAJILI VIJANA,KAZE ATOA NENO

 MSHAURI Mkuu wa Yanga kuelekea kwenye mfumo wa mabadiliko, Senzo Mbatha amesema kuwa wameamua kuwaongeza vijana ndani ya timu ili kwenda na kasi ya soka la kisasa.

Yanga jana Januari 27 ilimtambulisha Nizar Khalifan kuwa kocha msaidizi akichukua mikoba ya Juma Mwambusi ambaye aliomba kujiweka kando kutokana na matatizo ya kiafya pamoja na Edem Mortotsi kuwa kocha wa viungo.

Khalifan alikuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya African Lyon ambayo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza na pia aliwahi kucheza timu ya Mtibwa Sugar pamoja na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars. 

Mbatha amesema:”Tunahitaji kuongeza thamani ya ubora katika benchi ndio maana wote ni vijana na hata kocha mkuu wetu ni kijana ili kuendana na soka la kisasa,”.

Kaze ambaye ni mkuu Kwenye benchi la ufundi amesema kuwa anaamini watu waliochaguliwa ni sahihi  na watafanya kazi kwa ushirikiano.

“Ninaona watu ambao wamechaguliwa ni  watu wazuri hivyo ni suala la kusubiri na kuona namna ambavyo tutaendelea kupambana,”.

Yanga kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ipo nafasi ya kwanza na pointi 44 baada ya kucheza mechi 18.

SOMA NA HII  YANGA WATAJA SABABU ZA KUCHUKUA UBINGWA WA SIMBA