Yanga SC

KOCHA YANGA:TUTAFANYA VIZURI NDANI YA LIGI NA KOMBE LA SHIRIKISHO

admin February 1, 2021 5:47 am


 EDEM Mortotsi kocha wa viungo wa Klabu ya Yanga amesema kuwa anaamini kuwa timu hiyo italeta ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho pamoja na mashindano mengine ambayo watashiriki.

Kocha huyo anaungana na Kocha Mkuu, Cedric Kaze ambaye ni raia wa Burundi kuwanoa vinara wa Ligi Kuu Bara, wakiwa na pointi 44 baada ya kucheza mechi 18.

 Tayari kikosi hicho kimeanza mazoezi Januari 25 kwa ajili ya maandalizi ya mechi zao ikiwa na ingizo jipya la wachezaji watatu kwenye dirisha dogo ambao ni Fiston Abdulazack, Saido Ntibanzokiza na Dickson Job.

Mortotsi amesema:”Nimeona kwamba wachezaji wana morali na kila mmoja anapenda kufanya vizuri ndani ya uwanja hivyo ni mwanzo mzuri kwetu na wachezaji pia.

“Imani yangu ni kwamba tutakuwa na mwendo mzuri na tutaweza kufikia malengo ambayo tumejiwekea hivyo mashabiki wazidi kutupa sapoti,” .

AZAM FC KUKIPIGA DHIDI YA TP MAZEMBE GOMES AWAKAZIA MAZEMBE, ATAJA SABABU ZA SARE NA KUSEPA NA KOMBE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply