Home Simba SC SIMBA YASEPA NA POINTI TATU MBELE YA DODOMA JIJI,KITUO KINACHOFUATA AZAM FC

SIMBA YASEPA NA POINTI TATU MBELE YA DODOMA JIJI,KITUO KINACHOFUATA AZAM FC


DIDIER Gomes,  Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wachezaji wake wamepambana kusaka pointi tatu muhimu mbele ya Dodoma Jiji, jambo ambalo wanahitaji pongezi. 

Ikiwa Uwanja wa Jamhuri Simba imeshinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji kwenye mchezo wa Kiporo na kusepa na pointi tatu.

Bao la kwanza kwa Simba lilipachikwa na Meddie Kagere dakika ya 30 likawekwa usawa na Cleophance Mkandala dakika ya 36 ambaye alionyeshwa kadi ya njano kwa kushangilia akiwa ametoa jezi.

Bernard Morrison ambaye aliweza kuanza kwenye mchezo wa kwanza wa Gomes ndani ya Simba katika Ligi Kuu Bara alipachika bao ushindi dakika ya 66 kwa pasi ya Perfect Chikwende. 

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 38 ikiwa imeachwa kwa pointi 6 na watani zao wa jadi Yanga wenye pointi 44 wakiwa nafasi ya kwanza.

Gomes amesema:”Wachezaji wamepambana kutafuta pointi tatu wanahitaji pongezi hesabu zetu ni mchezo wetu ujao wa Ligi Kuu Bara, “.

Februari 7 Simba itashuka Uwanja wa Mkapa kusaka pointi tatu mbele ya Azam FC inayonolewa na George Lwandamina. 

Mbwana Makata, Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji amesema kuwa wachezaji wake wamecheza kwa nidhamu licha ya kupoteza mchezo wa leo.

SOMA NA HII  KUELEKEA MSIMU UJAO...DEO KANDA AFUNGUKA ISHU YA KURUDI TENA SIMBA....AITAJA YANGA....