kimataifa

NEYMAR ATAKA KUKAA MUDA MREFU NDANI YA PSG NA MBAPPE

admin February 9, 2021 8:47 am


 MSHAMBULIAJI wa Klabu ya PSG, Neymar Jr amesema kuwa atabaki ndani ya kikosi hicho pamoja na nyota mwenzake Kylian Mbappe.

Imekuwa ikielezwa kuwa nyota hao wapo kwenye mpango wa kusepa ndani ya PSG ili kupata changamoto mpya.

Mbappe amekuwa akitajwa kuwekwa kwenye rada na Liverpool huku Neymar Jr akitajwa kurejea ndani ya Klabu ya Barcelona.

Neymar amesema kuwa wanahitaji kubaki ndani ya timu hiyo kwa muda mrefu ili kuona wanapata mafanikio ndani ya timu hiyo.

“Wachezaji wote tunapenda kuona kwamba tunafikia mafanikio ambayo tunayatafuta na itapendeza ikiwa tutabaki ndani ya timu hii kwa muda mrefu.

“Mambo mengi yamebadilika, nina furaha kuwa hapa na ninapenda kuwa hapa kwa sasa ninaamini kwamba hata Mbappe naye pia anafuraha atafanya kama mimi,” .


SIMBA WAMEPAA NA VISIT TANZANIA NA WENGINE WAIGE KAZE: WAMEBADILI TARAHE..LAKINI KIPIGO KWA SIMBA KIPO PALEPELE..!!!

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply