news

SIMBA,YANGA WAHITIMISHA CHEMSHA BONGO YA SPOTI XTRA

admin February 9, 2021 3:47 pm


ILE Chemsha Bongo iliyokuwa inaendeshwa na Gazeti la Spoti Xtra ambayo ilikuwa inawapa fursa wasomaji wa gazeti hilo kujishindia zawadi mbalimbali kama seti za vyombo, microwave, friji na vyombo mbalimbali vya nyumbani, imefikia tamati leo Jumanne baada ya washindi watatu kujishindia zawadi mbalimbali.


Washindi hao watatu waliohitimisha chemsha bongo hiyo na kukabidhiwa zawadi zao jana Jumanne kwenye Ofisi za Gazeti la Spoti Xtra zilizopo Sinza Mori jijini Dar ni Maua Mutabazi ambaye ni shabiki wa Simba kama ilivyo kwa Gaisa Hamis pamoja na Mwanaidi Ally, shabiki mkubwa wa Yanga.


Spoti Xtra kwa kushirikiana na Vunja Bei Mobile Shop ilianzisha chemsha bongo hiyo ambayo ilidumu kwa takribani miezi mitatu kuanzia Desemba mwaka jana hadi Februari mwaka huu, lengo kubwa ni kuwaleta karibu wasomaji wake huku pia ikiwa ni ujio wa Gazeti la Spoti Xtra Jumanne.


Kwa sasa Gazeti la Spoti Xtra linapatikana mtaani mara tatu kwa wiki, JUMANNE, ALHAMISI na JUMAPILI kwa bei ya Sh 500 tu.


KAMA GATOGATO AMEWEZA, KAYOKO NA SASII HAWAWEZI KUSHINDWA MABINGWA WATETEZI WA KOMBE LA SHIRIKISHO KUKUTANA NA AFRICAN LYON

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply