Taifa Stars

RASMI NDAYIRAGIJE AFUTWA KAZI STARS

admin February 11, 2021 10:47 am

 


SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF), limetangaza rasmi kuachana na kocha wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Etienne Ndayiragije kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Akizungumzia uamuzi huo, Ofisa habari wa TFF Clifford Marion Ndimbo amesema wanamshukuru kocha huyo, na tayari mchakato wa kumsaka mbadala wake umeanza ambapo atatangazwa muda wowote kuanzia sasa.

“Baada ya kikao cha pamoja na kocha Etienne Ndayiragije, pande zote mbili zimefikia makubaliano rasmi ya kuvunja mkataba.

“Tunamshukuru kocha Ndayiragije kwa kazi yake kipindi chote alichoifundisha Stars, mchakato wa kumtangaza mbadala wake unaendelea na atatangazwa muda wowote kuanzia sasa,”

KAMA UNAMPENZI HII INAKUHUSU ..PATA ZAWADI YA VALENTINE NA UUMPENDAYE …SIMPLE TU NA Infinix… UJUMBE WA SIMBA KWA AS VITA YA DR CONGO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply