Kocha JKT Tanzania
Michezo Bongo

Kocha JKT Tanzania Afunguka Sababu za Mwanzo Mbaya Ligi Kuu Bara

Vardo September 1, 2026 9:27 am

MWANZO wa kusuasua wa kikosi cha JKT Tanzania katika msimu mpya wa Ligi Kuu Bara umemfanya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Ahmad Ally, kuweka wazi mambo mazito yanayowarudisha nyuma, huku akitaja ugumu wa ratiba kuwa mtihani mkubwa zaidi.

JKT Tanzania imeanza msimu kwa kusuasua ikikusanya pointi 4 pekee kati ya 12 katika michezo yake nne ya kwanza:

  • JKT Tanzania 1-1 TRA United (Nyumbani)

  • Polisi Tanzania 2-0 JKT Tanzania (Ugenini)

  • Yanga SC 4-0 JKT Tanzania (Ugenini)

  • JKT Tanzania 2-1 Namungo FC (Nyumbani)

Akitathmini mwenendo huo, Kocha Ally ameeleza kuwa kuna utofauti mkubwa kati ya msimu huu na msimu uliopita, akisisitiza kuwa changamoto zinazowakabili kwa sasa ziko nje ya uwezo wa benchi la ufundi.

1. Ugumu wa Ratiba na Uchovu wa Safari

Kocha Ally amebainisha kuwa timu hiyo inalazimika kusafiri umbali mrefu barabarani kwa basi bila kupata muda wa kutosha wa kupumzika.

“Tunasafiri umbali mrefu na ratiba inatubana kucheza kila baada ya saa 72. Safari zingine zinachukua hadi saa 24 njiani. Wachezaji wanafika wakiwa wamechoka sana na kuingia uwanjani, wakati wapinzani wetu mara nyingi wanakua wakiwa wamepumzika na wana nguvu za kutosha,” alisema Kocha Ally.

2. Muda Mchache wa Pre-Season (Maandalizi)

Mbali na ratiba, kocha huyo aliongeza kuwa timu haikupata muda wa kutosha wa kujiandaa vizuri kabla ya msimu kuanza, jambo linaloathiri utimamu wa mwili (fitness) wa wachezaji wengi.

“Kipindi cha maandalizi kilikuwa kifupi sana ukilinganisha na msimu uliopita. Ndio maana wachezaji wanaonekana kutokuwa sawa kimwili. Hata hivyo, tunapambana kila siku kurekebisha makosa haya ili turudi kwenye ubora wetu,” alihitimisha.

Matokeo Yanga vs Fountain Gate 2-0: Yanga Yaendeleza Ubabe Ligi Kuu Rekodi ya Edgar William: Kiboko ya TRA United Ligi Kuu Bara