Steve Barker Libasse Gueye
Simba SC

Barker Afichua Sababu ya Kumtoa Libasse Gueye Dhidi ya Geita Gold

Vardo September 1, 2026 10:03 am

Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, ameweka wazi sababu ya kumtoa uwanjani mshambuliaji wake wa pembeni, Libasse Gueye, wakati wa mchezo dhidi ya Geita Gold FC. Barker amesisitiza kuwa uamuzi huo haukutokana na kushuka kwa kiwango cha mchezaji huyo, bali ulikuwa mkakati wa kumlinda kutokana na ratiba ngumu inayowakabili.

Simba SC iliendeleza wimbi lake la ushindi baada ya kuichapa Geita Gold FC kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, na kufikisha ushindi wa tano mfululizo katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Sababu ya Kumtoa Libasse Gueye

Barker alieleza kuwa Gueye alikuwa akionyesha kiwango kizuri uwanjani, lakini benchi la ufundi liliona kuna haja ya kumpunguzia dakika za kucheza ili kumhifadhi kwa ajili ya mechi zijazo za ushindani mkubwa.

“Ulikuwa mchezo mzuri sana na wenye ushindani. Tulidhibiti mchezo, tukatengeneza nafasi za kutosha na kuzitumia vizuri. Kwa ujumla ilikuwa ni performance nzuri tukiwa na mpira na hata bila mpira,” alisema Barker.

Mipango ya Ligi ya Mabingwa Afrika

Ingawa Simba SC imeanza msimu vizuri kwa kushinda mechi tano mfululizo, kocha huyo ameeleza kuwa bado wana kazi kubwa ya kufanya ili kufikia kiwango bora zaidi anachokitarajia.

Baada ya kumaliza majukumu ya ligi ya ndani kwa sasa, nguvu zote za Simba SC zinaelekezwa kwenye maandalizi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ya kurejea kuwakabili Azam FC.

Barker alitimazia kwa kueleza umuhimu wa kusimamia uzito wa kazi kwa wachezaji wa winga:

“Winga ni wachezaji wanaotumia nguvu nyingi. Libasse anacheza kwa kasi na mara nyingi anawachukua mabeki moja kwa moja, hivyo lazima tusimamie dakika zao uwanjani. Ni uamuzi wa makusudi kumhifadhi kwa ajili ya mchezo mkubwa unaokuja na kupunguza hatari ya majeraha, kwani msimu ni mrefu.”

Farouk Komara Aangaza Yanga: “Sitaki Maslahi Binafsi, Ni Timu Kwanza!”