Simba SC

ISHU YA MABAO MATANO KIMATAIFA, MANULA APATA KIGUGUMIZI

admin February 12, 2021 7:47 am


 KIPA namba moja wa Klabu ya Simba, Aishi Manula amepata kigugumizi kuzungumzia kichapo cha mabao matano yaliyopita kwenye mechi zao za kimataifa.


Manula alikuwa langoni kwenye mechi tatu za ugenini msimu wa 2018,  ambapo jumla alikusanya mabao 12 ilikuwa Januari 19,2019, AS Vita 5-0 Simba,Februari 2,2019 Al Ahly 5-0 Simba na Machi 9,2019, JS Saoura 2-0 Simba.

Leo Februari 12, Simba itakutana tena na wapinzani wao AS Vita ambao waliwafunga Simba mabao 5 wakiwa Congo ila walipokuja kwa Mkapa, walinyooshwa kwa kufungwa mabao 2-1.

Manula amesema kuwa mechi za nyuma tayari zimeshapita wanachofanya wao ni kutazama upya mechi zao za mbele.

“Kuhusu hilo weka pembeni kwanza kwa kuwa mechi za nyuma zimepita na sasa tunatazama mechi zetu za mbele, kikubwa ni kuona kwamba tunapata matokeo chanya, mashabiki watuombee,” amesema.

TUCHEL AITAKA SAINI YA ERIKSEN WA INTER MILAN MASTAA YANGA WALA KIAPO KUIUA MBEYA CITY KESHO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply