Ligi Kuu

DUH! MVUA YAIPONZA KMC ISHINDWE KUPATA USHINDI

admin February 14, 2021 10:47 am


UONGOZI wa Klabu ya KMC umesema kuwa Uwanja wa Nelson Mandela ulikuwa kikwazo kwao kupata pointi tatu kwa kuwa walifanya mazoezi ukiwa umejaa maji jambo lililowapa ugumu kupata matokeo.

Kwenye mchezo wa mzunguko wa Ligi Kuu Bara uliochezwa juzi, KMC ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 na Prisons na kuwafanya waache pointi tatu jumla ugenini.

 Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa walishindwa kupata pointi tatu kutokana na miundombinu kutokuwa rafiki kwao licha ya ubora wa kikosi chao.

β€œTulikuwa ugenini hatukuweza kupata ushindi ipo wazi licha ya kwamba kikosi chetu ni imara na kinacheza kwa kujiamini.Hatujakata tamaa tunarejea kujipanga dhidi ya Mwadui FC,Februari 16.

β€œUwanja haukuwa mzuri, tangu tumefika mvua zilikuwa zinanyesha na uwanja ulikuwa umejaa maji jambo ambalo lilifanya wachezaji washindwe kuonyesha kiwango kizuri, wapinzani wetu wamepata nafasi na wamezitumia hivyo wanastahili pongezi,”.

Mchezo wa wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Uhuru, KMC iliyo nafasi ya 6 na pointi 25 ilishinda mabao 2-1 hivyo Prisons iliyo nafasi ya 7 na pointi 25 imelipa kisasi nyumbani kwa ushindi wa mabao 2-1.

SIMBA YAPIGA HESABU KUMALIZANA NA BIASHARA UNITED YANGA:HATUNA PRESHA, TUTAPAMBANA KUFIKIA MALENGO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply