Simba SC

SIMBA YAPIGA HESABU KUMALIZANA NA BIASHARA UNITED

admin February 14, 2021 9:47 am


 UONGOZI wa Simba umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United ambao unatarajiwa kuchezwa Februari 18, Uwanja wa Karume, Mara.

Simba kwenye msimamo ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 39 inatarajiwa kukutana na Biashara iliyo nafasi ya nne na pointi zake 32 baada ya kucheza jumla ya mechi 19 ndani ya ligi.

Leo inarejea kutoka DR Congo ambapo imetoka kucheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya makundi na ilishinda bao 1-0 dhidi ya AS Vita.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya ushindani ndani ya ligi na kesho kikosi kitaingia kambini kabla ya kuwafuata wapinzani wao.

“Kesho kikosi kitaripoti kambini rasmi kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Biashara United, tunatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu ila bado kuna jambo letu tunahitaji kutimiza.

“Mashabiki wazidi kutupa sapoti kwani malengo yetu ni kuona kwamba tunafanya vizuri kwenye ligi pamoja na Ligi ya Mabingwa.

“Tunatambua kwamba Biashara ni timu bora na ina wachezaji wazuri hivyo tunawaheshimu ila tutaingia ndani ya uwanja kusaka pointi tatu,” amesema.

MAJERAHA KUMUWEKA NJE POGBA NDANI YA MANCHESTER UNITED DUH! MVUA YAIPONZA KMC ISHINDWE KUPATA USHINDI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply